![]() |
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la James Juma (25-30) mvuvi ameuawa
kwa kukatwa panga sehemu za usoni na mkono wa kulia mara baada ya kubainika ana
mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtu katika kijiji cha Nkome mkoani Geita.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Geita Leonard Paul amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja na nusu usiku katika kitongoji cha Jakalanda kijiji cha Nkome wilayani Geita ambapo James Juma
mkazi wa kijiji jirani cha Ihumilo aliuawa kwa kukatwa panga na Makaranga
Charles(30-35).
Amesema tukio hilo limetokea baada ya Makaranga kumhisi James Makaranga kuwa anatembea na
mkewe Regina Revocatus kwa muda mrefu ndipo mtuhumiwa aliamua kuweka mtego na
kumkuta marehemu katika mazingira yaliyomfanya
kutekeleza mauaji hayo.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Lucas Mbodi ameeleza kuwa hadi sasa mwili wa
marehemu wameuchukua na kumpeleka kwake kijiji cha Ihumilo ambapo mazishi
yatafanyikia huko kwa mkewe.
Hadi hivi sasa mtuhumiwa na
mkewe wametoroka na hawajulikani walipo na jeshi la polisi linaendelea
kuwatafuta watuhumiwa hao.
Na Valence Robert-Geita
Post a Comment