Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mwajuma
Hamisi, mkazi wa Yombo Vituka kwa kosa la kukutwa na ngozi mbili za chui
kinyume cha sheria, zenye thamani ya sh milioni 11.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,
Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema mwanamke huyo
alinaswa Januari 18, mwaka huu katika eneo la Yombo Vituka, Wilaya ya
Temeke.
Kova alisema mwanamke huyo alinaswa baada ya Ofisa Mhifadhi
Wanyamapori mkazi wa Ukonga, kutoa taarifa kituoni hapo kwamba kuna
mwananchi anauza ngozi za chui.
Alisema askari walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa na
walipompekua chumbani kwake, walimkuta na nyara hizo za serikali.
chanzo -Tanzania daima
Post a Comment