 |
Dua
ya kuuombea kheri mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa kundi la uchekeshaji
wa luninga la FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa jina la Mzee
Dude ilifanyika majira ya saa 9:00 nyumbani kwake Ilemela jijini Mwanza
ikiwa kabla ya mazishi yaliyofanyika jana jioni majira ya saa 10:00. |
 |
Awali kabla sala maalum ilifanyika. |
 |
Waigizaji
mbalimbali wa sanaa mbalimbali wameshiriki akiwepo Mc. Katumba ambaye
anaonekana akiwa na wasanii wa kundi la BABATAN Itagata, Kafuku
Kahualanga na Mwanshum ambao walifanya kazi na marehemu kwenye kundi la
FUTUHI (kabla hawajajiengua) na wa kwanza kulia ni Tatu wa FUTUHI. |
 |
Ni
wakati wa kuusitiri mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa kundi la
uchekeshaji wa kundi la FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa
jina la Mzee Dude, katika makaburi ya Iloganzala wilayani Ilemela jijini
Mwanza. |
 |
Kwa
mapenzi mema na urafiki hata watoto wadogo walishiriki kuweka mchanga
kuusitiri mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa kundi la uchekeshaji wa FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa jina la Mzee Dude
aliyefariki juzi jioni majira ya saa 11 jioni |
 |
Katika mazishi hayo Beat Agenda iliwakilishwa naye DVJ Bavon (mwenye skafu na kofia kushoto). |
 |
Shekhe
wa wilaya ya Ilemela Shk. Mohamed Yusufu akitoa neno la barka kwa
waliohudhuria mazishi hayo |
 |
Baadhi ya watoto wa marehemu wakijumuika na wajukuu na marafiki wengine wa marehemu katika sala ya kuhitimisha maziko kifamilia. |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment