MTOTO APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA HUKO GEITA

Ikiwa ni  siku chache tu baada ya mtoto Geofry  kuibiwa siku ya krismas aliibiwa akiwa anasubiri wazazi wake kwenda kanisani hali hiyo imejitokeza tena mara baada ya mtoto mwingine aliyefahamika Peter Shakini (6) mkazi wa Katoro ameibiwa na kupelekwa kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea Desemba 30 mwaka jana baada ya kuchukuliwa na Majuto Kurwa kwa baiskeli kutoka nyumbani kwa mama yake mzazi aitwaye Semeni Makoye (25) .


Imeelezwa kuwa baadae mtuhumiwa aliyekuwa amemchukua mtoto huyo alirudi nyumbani kwa mama huyo akiwa hana mtoto na kumwambia kuwa alitekwa na watu wanne waliokuwa na gari aina ya Noah asiowafahamu na kupelekwa katika pori moja la Samina lililopo katika kata ya mtakuja wilayani Geita.

Mtuhumiwa huyo alisema akiwa katika pori aliteswa na baadae alipewa namba ya simu ambayo alielekezwa ampe mjomba wake aitwaye Maneno Makoye ndipo mtoto huyo ataachiwa.

Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa Majuto Kurwa kabla ya wizi wa mtoto huyo aliwahi kumfuata mama yake mdogo na kumwambia atembee naye kimwili lakini siku tu chache baada ya mama yake kukataa ndipo alipomchua mtoto kwa baiskeli na alirudi kwa mama wa mtoto alidai kuwa ametekwa na watu wenye gari aina ya noah na kumpora mtoto ambapo taarifa hizo zilitiliwa shaka na polisi na kumshikilia Majuto Kurwa na katika upelelezi ilibaini kuwa majuto alimiba mtoto na kumficha na ndipo alipokamatw mtuhumiwa mwenzake Makungu Panga(28) mkazi wa katoro.

Hata hivyo Majuto alipohojiwa zaidi baada ya kutolewa mahabusu alieleza kuwa mtoto huyo amefichwa kijiji cha chigunga tarafa ya Butundwe ambapo mama huyo akienda huko atamkuta hata ingawa hali  ya motto huyo  baada ya kupimwa alionekana amekutwa na UTI.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Leonard Paul amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa taratibu za kisheria zimeshaanza ili kubaini mtandao huo ili ukomeshwe mara moja na ameendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kubaini watu wa namna hii na kuwachukulia hatua za kisheria.


Na Valence Robert- Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post