Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele
mchezo wa marudiano wa daraja la kwanza kati ya Stand United na Kanembwa JKT
ulipangwa kuchezwa tarehe 1 mwezi Februari mwaka huu katika uwanja wa Ally
Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho hilo iliyotolewa tarehe
28 mwezi huu, na katibu mkuu wa wa shirikisho hilo Mwesigwa Selestine kwa timu
hizo mbili mchezo huo wa marudiano utapangiwa tarehe nyingine huku akizitaka
timu husika na wasimamizi wa mchezo huo wasiende katika kituo cha Tabora.
Na Isaac wa Edo,Shinyanga
Social Plugin