 |
Helikopta ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ikitua katika viwanja vya Shy-com Mjini Shinyanga jioni ya leo ambapo wakazi mbalimbali wa mkoa waShinyanga walikuwa wanawasubiri kwa hamu kubwa makamanda wa chama hicho wakiwemo viongozi wakuu wa Chama, watendaji kutoka Makao Makuu ya
Chama katika kutekeleza kampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB) inayoendeshwa katika mikoa yote nchini. |
 |
Viongozi wa chadema wakiingia katika viwanja vya Shy-com mjini Shinyanga baada ya kushuka kwenye usafiri wao wa anga.Miongoni mwa viongozi hao yumo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa ,Makamu
Mwenyekiti Zanzibar, Issa Saidi Mohamed, Mkurugenzi wa Mawasiliano na
Uenezi wa Chadema John Mnyika na
mbunge wa jimbo la Maswa mashariki lililopo mkoani Simiyu Sylvester Kasulumbayi
|
Awali mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Bi Siri Yasin akimkaribisha
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare ili azungumze na wananchi wa shinyanga katika mkutano huo ambapo alisema CHADEMA sasa ipo katika
uwanja
wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima
 |
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare akizungumza na maelfu ya wakazi wa Shinyanga waliohudhuria mkutano huo katika viwanja vya shy-com ambapo pamoja na mambo mengine chama hicho kinatumia vita kupitia angani ili kuwafikia
wananchi wengi
kadri itakavyowezekana,kuanzia kwenye vitongoji,mitaa,vijiji, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wake wa ndani
kuanzia ngazi ya mashina, uchaguzi mdogo wa madiwani nchini
utakaofanyika Februari 9, mwaka huu pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
|
 |
Mbunge wa jimbo la Maswa mashariki lililopo mkoani Simiyu Sylvester Kasulumbayi akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wasukuma kutumia wingi wao kuiondoa CCM kuipokea CCM ni kupokea majanga
 |
Mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi CHADEMA John Mnyika akizungumza katika mkutanoa ambapo alizungumzia suala la
Watanzania na umiliki wa rasilimali zao ambazo kwa sasa zinaonekana
kuwanufaisha wageni, watawala na watu wenye mahusiano na watawala, pia hali
ya ugumu wa maisha inayozidi kuwakabili wananchi ikiwa na uhusiano na uongozi
mbovu unaokumbatia ufisadi na sera zilizoshindwa.Mnyika alitolea mfano wa migodi iliyopo nchini kutowanufaisha wananchi huku wageni wakifaidika na kuacha mashimo.Alisema bado miaka 7 madini katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama yataisha lakini pia miaka 15 mgodi wa almas wa Mwadui utafungwa kutokana na madini kuisha katika mgodi huo |
|
 |
Viongozi mbalimbali wa Chadema jukwaa kuu wakifuatilia hotuba ya John Mnyika |
 |
Wananchi wa Shinyanga wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya John Mnyika |
 |
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa
akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwatahadharisha vigogo wa Serikali wanaoiba fedha za umma kuwa, CHADEMA itawashtaki
na kuwafilisi iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mwaka 2015.
Alisema chama hicho kikishinda dola, kitaboresha
maslahi kwa watumishi waadilifu lakini mafisadi wanaotafuna fedha za Serikali
watapata wakati mgumu kwani hakitakuwa na huruma na viongozi wasio waadilifu hata kama wanatoka ndani ya CHADEMA.
|
 |
Maelfu wa wakazi wa Shinyanga wakiwa wamenyoosha mikono baada ya kuulizwa na katibu mkuu wa chadema kama wanaunga jitihada zinazofanywa na chama hicho ikiwa ni pamoja kumwajibisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe aliyekimbilia mahakamani ili kunusuru uanachama wake |
 |
Dkt Slaa akimkaribisha Makamu
Mwenyekiti chadema Zanzibar, Issa Saidi Mohamed ili azungumze na wakazi wa Shinyanga kwa mara ya kwanza katika mkutano huo baada ya yeye kumaliza kutoa hotuba yake |
 |
Makamu
Mwenyekiti Chadema Zanzibar, Issa Saidi Mohamed akizungumza katika Viwanja vya Shy-com ambapo alisema chadema wamejipanga ipasavyo katika kuhakikisha kuwa CCM inaondolewa madarakani na kwamba Chadema katika mapambano hayo wameanza na mungu,wanaendelea na mungu na watamaliza na mungu katika kuhakikisha kuwa ukombozi unapatikana na kwamba silaha pekee ya kuiondoa CCM ni kuwa na kitambulisho cha mpiga kura hivyo akatumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuhamasishana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura |
 |
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakisikiliza hotuba ya Makamu
Mwenyekiti Chadema Zanzibar, Issa Saidi Mohamed.
CHADEMA hivi sasa ipo katika uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni
Pamoja Daima, Timu zake zinashambulia kutokea timu hizo zinajumuisha viongozi
wakuu wa Chama, watendaji kutoka Makao Makuu ya Chama, Wajumbe wa Kamati Kuu,
Viongozi wa Kanda, Mikoa, Wilaya, Majimbo, Kata, Vijiji na Vitongoji pamoja na
wabunge wote wa CHADEMA katika maeneo husika.
CHADEMA inatumia operesheni hiyo kuwandaa umma wa Watanzania juu ya masuala
kadhaa muhimu kwa hatma ya nchi yao kama vile Mjadala wa rasimu ya pili ya
katiba mpya- Bunge Maalum la Katiba Mpya Wakati huu ambapo Watanzania
wanasubiri vikao vya Bunge Maalum la Katiba.
Lakini pia oparesheni hiyo inalenga Kuhusu uboreshwaji
wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya pamoja na Uchaguzi wa ndani ya chama
ambao hadi sasa unaendelea katika ngazi ya msingi nchi nzima hatimaye ngazi ya
taifa | | |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment