MCHUNGAJI MTOTO AFARIKI BAADA YA KUZAMA KWENYE MTO

NB-Siyo mto alimozama mchungaji wa ng'ombe
 Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mihayo  Mhuri (12)  Mkazi wa Center  Maria  Kata ya Kakese  Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi  amefariki dunia  baada ya kuzama kwenye  maji ya mto wakati  akiwa  akiogelea kwenye maji akichunga ng’ombe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  tukio hilo  lilitokea juzi majira ya saa tano na nusu asubuhi  katika mto wa Katuma   Wilayani Mpanda.

Siku hiyo ya tukio marehemu  akiwa  na mdogo wake  aitwaye  Wakasoro  Nhuri 7 waliondoka  nyumbani kwao na kuelekea  kuchunga ng’ombe  katika maeneo  ya Karibu na mto Katuma.

 Wakiwa  maeneo hayo marehemu  alipatwa na jasho  na ndipo alipoamua  kuvua nguo  na kuingia  ndani ya mto Katuma kwa ajili ya kuogelea  na kumwacha  mdogo wake  akiwa kando ya  Mto.

Kamanda Kidavashari  alisema  wakati  marehemu  akiendelea kuoga  alizidiwa  na maji  na kuanza  kuzama  chini ya maji ya mto huo  kitendo ambacho kilimshitua mdogo wake ambae  alikuwa  kando ya mto huo.

Mdogo  wake  alianza kupiga kelele  za kuomba msaada  kwa watu   huku akilia na watu walikusanyika katika eneo hilo na mdogo wa marehemu aliwaeleza kuwa kaka yake amezama kwenye maji ya mto huo wa Katuma.

Kidavashari alieleza watu hao walianza jitihada za kumtafuta marehemu  baada ya  kitambo kidogo  waliweza  kuupata mwili wa  marehemu  ukiwa umekwama  kwenye Gogo pembeni ya mto  huku akiwa ameshafariki dunia.

Na  Walter M guluchuma
Katavi yetu blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post