Kwa mara ya Kwanza kutokea Shinyanga!!! WAMILIKI NA MAMENEJA WA SHULE NA VYUO VISIVYO VYA SERIKALI WAKUTANA SHINYANGA

Aliyesimama na mwenyekiti wa shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali kutoka kanda za magharibi bwana Jerry Nyabululu akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga katika mkutano 
wa wanachama wa shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali kutoka kanda za magharibi inayojumuisha mikoa ya Shinyanga ,Simiyu na Tabora,kanda ya ziwa magharibi inayoundwa na mikoa ya Kagera na Kigoma pamoja na kanda ya ziwa inayoundwa na mkoa wa Geita,Mwanza na Mara .Mkutano huu ni wa kwanza kufanyika mkoani Shinyanga
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika ukumbi wa mikutano wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hapo jana.Mkutano huo wa mameneja na wamiliki wa shule binafsi umefanyika kwa siku mbili (Alhamis na Ijumaa) katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga lengo ni kujadili masuala mbalimbali kuhusu maendeleo ya elimu hapa nchini

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine
aliwaasa wamiliki na mameneja wa shule ambazo siyo za serikali kupunguza gharama ikiwemo ada za shule ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa wanafunzi katika shule hizo.
Alisema pengine hawapati wanafunzi wengi kutokana na ada za shule binafsi kuwa kubwa ukilinganisha na kipato cha wananchi.Mkuu huyo wa mkoa pia aliwapongeza wamiliki wa shule za watu binafsi kuendelea kufanya vizuri katika sekta ya elimu mfano katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana shule ya kwanza ni Rocken Hill ya wilayani Kahama mkoani Shinyanga na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao katika kuboresha elimu hapa nchini huku akiwaomba  pia kuboresha miundo mbinu katika shule ili kujenga mazingira mazuri kujifunzia kwa wanafunzi


Aliyesimama ni mwakilishi wa kamishina wa elimu nchini bi Hadija Mcheka akizungumza katika mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine alisema ada kubwa katika shule za watu binafsi zinakatisha tama kwa wananchi hivyo kuwaomba wamiliki wa shule hizo kuangalia namna ya kupunguza gharama hizo ili wanafunzi wengi wapate elimu hapa nchini.

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mawili matatu katika mkutano huo.Washiriki wa mkutano huo kupitia risala iliyosomwa na mwenyekiti wa shirikisho hilo kanda ya Magharibi Jerry Nyabululu ambayo ilitaja miongoni mwa changamoto wanayokutana nayo ni ukosefu wa wanafunzi katika baadhi ya shule na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupata wanafunzi katika shule zao za binafsi.Lakini pia walisema kumekuwa na ubaguzi katika suala la ukaguzi katika shule ambapo shule za watu binafsi zinafuatiliwa sana tofauti na shule za serikali hali ambayo walisema inaashiria ushindani kati ya shule za watu binafsi na serikali.Washiriki wa mkutano huo walisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto ya kukosa wanafunzi katika shule zao pamoja na serikali kutowaamini walimu wa shule hizo katika suala la mitihani(usimamizi wa mitihani)
Picha ya pamoja baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga kufungua rasmi mkutano huo wa siku mbili mjini Shinyanga.Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga alitumia fursa ya mkutano huo kuwapongeza wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali kwa kuendelea kuwa wadau wakubwa wa mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa(BRN) ambapo hata katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne mwaka jana wameonesha mfano mzuri.Mfano katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana katika shule za kanda hizo tatu Shule ya Rocken Hill ya Kahama imechukua nafasi ya kwanza,shule ya Kwema ya Kahama imechukua nafasi ya nne kitaifa,Bariadi Allience ya Mkoa mpya wa Simiyu imechukua nafasi ya 9 na Mwanza Allience ambayo imechukua nafasi ya 15 kitaifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post