Kimenuka!!! MADIWANI WA CHADEMA SHINYANGA MJINI WAWASHA MOTO KWA MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE



Ikiwa ni siku chache tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini kufanya mkutano wa hadhara mjini Shinyanga na kusema kusema kuwa madiwani wa CHADEMA wamekuwa mzigo katika jimbo lake, Madiwani wa chama cha Demokrasia na Maendelao CHADEMA katika manispaa ya shinyanga wamekanusha tuhuma zilizotolewa dhidi yao na mbunge wa jimbo la shinyanga mjini Stephen Masele kuwa madiwani wa chama hicho ni mizigo katika jimbo lake kutokana na kushindwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

Madiwani hao wa CHADEMA waliyasema hayo jana mjini Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara ambao waliuitisha kwa lengo la kujibu tuhuma ambazo amekuwa akitoa mbunge huyo mbele ya wananchi mfano katika mkutano wa mwezi uliopita katika viwanja vya mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga Masele alisema kwamba madiwani wa CHADEMA katika jimbo la Shinyanga mjini wamekuwa mzigo kwa kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zahanati.

Madiwani hao wamesema wao sio mizigo  kutokana na kwamba katika kata zao  tayari wameshawaletea maendeleo wananchi lakini mbunge huyo kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM amekuwa akiwachafua  kwenye mikutano yake ya hadhara badala ya kuangalia changamoto gani wanazokabiliana nazo madiwani hao.

Diwani wa kata ya Masekelo Zacharia Martin amesema mtu unapochaguliwa kuwa mbunge unatakiwa kuwasikiliza madiwani wote pamoja na kutatua changamoto zao kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi na siyo  kuwabagua kama anavyofanya Mbunge huyo wa Shinyanga mjini na kuwasema vibaya madiwani wa Chadema katika majukwaa kwamba hawafanyi kazi.

Martin alisema licha ya mbunge huyo kumpatia mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya kujenga zahanati katika kata yake lakini imeshindikana kutokana na eneo linalotakiwa kujengwa wananchi bado hawajalipwa fidia hivyo kumwia vigumu kutekeleza mradi huo.

Naye Diwani wa kata ya Ndala John Sungura aliyekuwa anatuhumiwa kula mifuko mia moja ya soko kuu Ndala amesema tangu achaguliwe kuwa Diwani hajawahi kumuona mbunge huyo akihudhuria hata siku moja kwenye kikao  cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo ndio  maana  hata miradi mingine ya maendelo anakuwa haijui pamoja na migogoro hiyo ya ardhi  na kusemakuwa anatakiwa kuwa anahudhulia kwenye vikao hivyo ilikujua madiwani wake wanafanya nini



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post