Askari polisi kujeruhiwa kwa risasi!!! KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA AZUNGUMZA KILICHOJIRI


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kuhusu tukio la askari kujeruhiwa kwa risasi

Dkt Fredrick Mlekwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake


Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema tukio la askari wake aitwaye David Alfred (25-30)kujeruhiwa kwa risasi limetokea jana majira ya sa 12 na nusu jioni wakati askari huyo akikagua silaha aina ya SMG katika ghala la silaha katika  kambi ya jeshi la polisi mjini Shinyanga ili aingie kazini.

Amesema wakati askari huyo akikagua silaha hiyo ghafla risasi ilifyatuka na kumjeruhi chini ya bega la mkono wa kushoto hali iliyopelekea akimbizwe katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.

Amesema tukio hilo ni bahati mbaya tu huku akiwataka askari polisi kuwa makini na kujali usalama wao kwanza kabla na wakiwa kazini.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri anaongea, vizuri  na kwamba kufuatia tukio hilo askari huyo amepata majeraha katika sehemu za kifuani na mkono wa Kushoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post