Breaking News!! WANAFUNZI WANNE WAFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA GARI WAKATI WAKIKIMBIA MCHAKAMCHAKA HUKO MTWARA

Habari za hivi punde zilizoufikia mtandao huu wa malunde1.blogspot.com zinasema kuwa Wanafunzi wanne Wa shule ya sekondari Mustapha Sabodo mjini Mtwara wamekufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Benzwakiwa kwenye mchakamchaka asubuhi ya leo.

Tukio hjilo limetokea leo majira ya saa asubuhi wakati wanafunzi hao wakikimbia mchaka mchaka.

Chanzo cha ajali hiyo kinatokana na gari dogo aina ya Benzi kumgonga mwanafunzi mmoja aliyekuwa kwenye mchakamchaka na katika hali ya taharuki ya mwenzao bila kuangalia nyuma ndipo lori  jingine likawagonga wanafunzi wengine na kusababisha mwanafunzi mmoja kufariki dunia papo hapo na wengine watatu wakifariki hospitali wakati wakipatiwa matibabu huku majeruhi wakiwa 20.


Dreva wa Benzi amejisalimisha kituo cha polisi Mtwara lakini Yule wa Lori amekimbia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post