WATU WATATU WAPIGWA NA RADI MKOANI GEITA,YUMO MTOTO WA MIAKA SABA


Watu watatu akiwemo mtoto wa miaka saba wamejeruhiwa kwa kupigwa na radi katika sehemu mbalimabali za miili yao katika kijiji cha Nyakafuru kata ya Nayakafuru tarafa ya Masumbwe wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Leonard Paul  amesema tukio hili limetokea Desemba 13 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kijiji hicho ambapo watu hao watatu walipigwa radi.

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Paulo  Lwelwe(39) bi Mwamba Paulo(18)  na  mtoto aitwaye Kiumbe Paulo(7) ambao wote walipigwa na radi wakati wakiwa nyumbani kwao wakati mvua ikinyesha katika kijiji  hicho.

Kamanda Paulo amesema majeruhi wote wamelazwa katika kituo cha afya cha Masumbwe kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Na Valence Robert -Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post