Viatu vya Mandela hivi hapa!!! SOMA HAPA HABARI FUPI KUHUSU SIKU MAMA VICKY NSILO SWAI ALIPORUDISHA (BUTI) VIATU VYA MANDELA


 Rais wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.

Mzee Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. 

Viatu hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia)   Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerzani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.
 Rais Kikwete akimtambulisha Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere kwa waombolezaji wakati wa shughuli ya mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu Afrika kusini Desemba 15 mwaka huu
 Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya Mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu
Mama Vicky Nsilo Swai akishangiliwa na waombolezaji kwenye mazishi ya Mzee Mandela wakati Rais Kikwete alipomtambulisha na kueleza historia ya jinsi alivyomkaribisha Madiba nyumbani kwake na kumtunzia viatu vyake, simulizi ambayo ilimsisimua kila mtu aliyekuwepo ukumbini hapo na mamilioni waliokuwa wanaangalia tukio hilo live dunia nzima.
Maandishi ya Mzee Mandela kwa Mama Vicky Nsilo Swai aliyoyaandika kwenye kitabu alichompa kama zawadi baada ya kurudishiwa viatu vyake mwaka 1995.
chanzo-michuzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post