Unyama mtupu!!! FAMILIA ILIYOVAMIWA NA KUPORWA RAMBI RAMBI ZA MSIBA MKOANI GEITA YASIMULIA TUKIO ZIMA, WALIFUNGWA KAMBA NA KULAZWA KIFUDI FUDI MKE AKIWA UCHI WA MNYAMA

Familia ya mzee Luhemeleja mkoani Geita iliyovamiwa kisha kuporwa pesa za rambi rambi kisha watuhumiwa kuchomwa moto wiki iliyopita

Mzee John Luhemeleja akiwa katika hospitali ya wilaya ya Geita akipatiwa matibabu

Familia ya mzee John Luhemeja [68]iliyovamiwa na kunyang’anywa rambirambi kiasi cha shilingi elfu 56 iliteswa kinyama baada ya kufungwa kamba yeye na mke wake Roza Kisinza (43)na kulazwa kifudifudi huku mwanamke akiwa mtupu na mme  akiwa amevaa bukta  pekee walimochukua pesa zile.

Akisimulia mkasa huo Mzee Luhemeja akiwa katika Hospital ya wilaya Geita Wodi No [8] alikolazwa akiuguza majeraha yake sehemu za kichwani na mdomoni amesema kuwa”akiwa amelala nyumbani kwake muda saa sita alisikia sauti ya mbwa anabweka nje ya nyumba yake akatoka nje akiwa na mkuki.

Alipotoka nje akakutana na kijana wake Kamuri John(6) anatoka kujisaidia akiwa amepigwa kofi na kuambiwa arudi ndani huku mzee akimrikwa tochi machoni na wezi  hao  na kushtukia anampigwa ubapa wa panga na kumuangusha hapo hapo .

Amesema wakiwa wanamsulubu walimwamuru atoe pesa alizonazo na yeye akipiga kelele ndipo mke wake aliposikia kelele hizo akatoka nje na kumkuta mme wake anapigwa akiwa ameangushwa chini………..

Ameongeza kuwa baada kutoka nje wezi hao waliwaamuru kurudi ndani wote huku wakiwa wamefungwa kamba kwenye mikono kwa nyuma na wakaambiwa kulala kifudifudi baada ya kipigo kuzidi mzee Luhemeja aliwaambia wafungue zipu kwenye kaptula ndipo wakakuta kiasi cha shilingi elfu 60 za rambirambi na kuzichukua.

Hawakuishia hapo lakini pia watu hao walimwamuru mke wa Luhemeja atoe pesa alizonazo naye akawanbia hana lini kipigo kilipozidi aliwaambia wachukue kwenye begi kuna shlingi elfu 5 aliyopewa jioni hio na waliokuja kumhani huku akiwa uchi wa mnyama na kamba zake….

Mzee Luhemeja ameendelea kusema kuwa baada ya kumaliza waliingia kwenya chumba cha mabinti walimokuwa wamelala na kuwataka watoe pesa ambapo walitoa kiasi cha shilingi elfu 80 na simu moja ya mkononi na majina yao ni Semeni John  miaka[23] Siwema John [16] na Kurwa John [14] wote walikuwa wamelala kwenye chumba hicho.

Baada ya watoto hao kutoa pesa na simu wakachukuliwa na kupelekwa kweye chumba cha wazazi wao waliokuwa wamelazwa kifudifudi nao wakaamuliwa kulala kifudifudi…..

Tukio hilo lilidumu kwa takribani saa moja majambazi hao waliamua kutoka na kuwafungia mlango kwa nje  huku wakiamuriwa wasipige kelele na wakipiga kelele wanawamaliza papo hapo.

Mzee huyo amesema baada ya muda mfupi mzee huyo aliomba afunguliwe kamba huku mke wake akisema asipige kelele watarudi kuwamaliza kwa vile mzee luhemeja alikuwa amechoka alimwambia mke wake acha watumalize tu ndipo mke wake akalegeza kamba zake na kujifungua na kisha kumfungulia mme wake……

Baada ya kufunguliwa waliwaita watoto wao waliokuwa nyumba nyingine  na kuwafungulia mlango na kumkuta Baba yao yuko hoi akiwa amekatwakatwa mapanga ndipo wakaita majirani wa karibu wakakusanyika na kupiga yowe huku mzee luhemeja akipelekwa Hospitali ambako amelazwa mpaka sasa akiendelea na matibabu……..

Baada ya yowe kuwa kubwa wananchi walikusanyika na kuanza kuwasaka waliohusika na kitendo hicho na walipowapata walianza kutajana mmoja baada ya mwingine na kufikia wananchi kuwapiga na kuwachoma moto huku wakisema wamechoshwa na vitendo hivyo”…………alisema mzee luhemeja.

Naye katibu wa Geita Legal Aid Center Bw,Elineema Charles anayeshughulika na utetezi wa haki za binadamu wilayani Geita amesema kuwa ni kitendo ambacho hakivumiliki cha watu kujichukulia sheria mikononi kwa kuua raia kama walivyofanya wakazi wa Geita kwa kuua watu hao watano kwani huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kwamba mahakama imenyang’anywa mamlaka yake ya kutoa haki.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Geita aliyefika kwenye eneo la tukio Bw Said Magalula amekeme vikali kitendo cha wananchi kujichukuli sheria mkononi na kulitaka jeshi la polisi kuwakamata wote walihusika na mauaji hayo ya kikatili ili sheria ichukue mkondo wake.


Na Valence Robert- Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments