Neema yaiangukia Timu ya Stand United!!! MGODI WA DHAHABU WA BUZWAGI WAIPATIA TIMU HIYO PENDWA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA MAMILIONI YA FEDHA ,MBUNGE WA SHINYANGA MJINI ,AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA MADINI AKABIDHI VIFAA HIVYO MJINI SHINYANGA

Ni katika eneo la Stendi ya mabasi maarufu kama stendi ya zamani ya mabasi yaendeyo mikoni,sasa ya wilayani.Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ndugu Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini(aliyevaa nguo nyeusi) akisalimiana na viongozi wa timu ya Stand United ambayo kimsingi inawakilisha mkoa wa Shinyanga.

Mheshimiwa Stephen Masele wa kwanza kutoka kushoto akiongea neno na mwakilishi wa meneja wa mkuu wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya African Barrick (ABG)- wa pili kutoka kulia bwana Amos John kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Stand United vyenye thamani ya shilingi milioni saba na laki 5.

Mwenyekiti wa timu ya stand united Amani Vicent akizungumza katika eneo la stendi ya mabasi mjini Shinyanga eneo ambalo ndiyo chimbuko la timu hiyo.Pamoja na mambo mengine mwenyekiti huyo aliiomba jamii kuwaunga  mkono bila kujali itikadi ya vyama vya siasa kwani timu hiyo siyo ya chama flani bali ni watu wotehivyo kuwaomba kuipa nguvu ili iweze kufikia malengo yake na kwamba wapo tayari kupokea msaada kutoka kwa mtu yeyote

Mbunge wa Shinyanga mjini  Stephen Masele (aliyevaa kofia) akiwa ameshikilia  jezi ,ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na mgodi wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Mheshimiwa Masele mbali na kuwa mbunge pia anasimamia mambo ya madini hapa nchini na msaada huo wa vifaa unatokana na ombi lake kwa mgodi huo ili kuisadia timu hiyo ambayo sasa ipo katika ligi daraja la kwanza

Wa nne kutoka kulia ni Mwakilishi wa meneja mkuu wa African  Barrick Gold Mine bwana Amos John akikabidhi viatu kwa ajili ya timu ya Stand United kwa mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele katika eneo la stendi ya mabasi mjini Shinyanga

Zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa timu ya Stand United likiendeshwa na mheshimiwa Masele linaendelea hizo ni jezi zingine zilizotolewa na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kwa timu hiyo

Hebu jaribishia kuvaa tuone!!!!Viongozi wa timu hiyo wakijaribu kuvaa jezi katika jukwaa mbele ya mbunge aliwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupata msaada huo na mgodi huo ukakubali kuwa mmoja wa wafadhili wa timu hiyo
Viongozi wa timu ya Stand United wakiwa wamevaa,kubeba na kushililia vifaa hivyo  kama vile jezi,mipira,mabegi,viatu,koni,bips.soks n.k walivyokabidhiwa na mbunge wao baada ya mgodi wa Buzwagi kukubali kuwa wafadhili.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa timu hiyo bwana Amani Vicent,wa pili ni katibu msaidizi wa timu hiyo bwana Araf Nassoro na wa tatu ni bwana Kennedy Nyange ambaye ni katibu mkuu wa Timu ya Stand United

 Mheshimiwa Masele akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu ya Stend United ambapo ameupongeza uongozi wa mgodi wa Buzwagi kwa kukubali kuwa wafadhili wa timu hiyo lakini pia kuwashukuru watu wote wanaoendelea kuiunga mkono timu lakini pia akatumia fursa hiyo kwa watu wote wenye mapenzi mema kuisaidia timu hiyo.Pamoja na mambo hayo yoteMasele alisema basi aliloahidi kuipatia timu hiyo liko tayari na watakabidhiwa hivi karibuni
Ni full shangwe !! Wapiga matarumbeta nao walikuwepo wakifanya yao eneo la stendi

Mwakilishi wa meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi bwana Amos John  akizungumza katika eneo la stendi ambapo alisema uongozi wa mgodi huo umefurahishwa na juhudi za timu hiyo na kutokana na timu hiyo kuwa mfano bora wa timu hapa mkoani Shinyanga,amesema wataendelea kutoa msaada kwa timu pale wanapohitaji na wao wakiwa kama wadau muhimu wa timu hiyo na hata timu nyingine itakayohitaji msaada wao wako tayari kusaidia ili kuinua kiwango cha michezo mkoani Shinyanga na nchi kwa ujumla.Aidha amesema miongoni mwa vifaa walivyokabidhi ni  jezi pea 2,viatu 45,bibs 30.koni 30 na mipira 20 na thamani ya vifaa vyote ni shilingi milioni 7 na laki 5.

Picha ya pamoja baada ya zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo likiwa limekamilika.Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na katibu mkuu wa timu hiyo bwana Kennedy Nyange timu hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi miongoni mwa changamoto hizo ni suala la chakula,usafiri,posho kwa walimu na wachezaji hivyo kutumia fursa hiyo kuziomba taasisi mbalimbali,wafanyabiashara,migodi ya madini iliyopo mkoani Shinyanga kuisaidia timu hiyo ambayo sasa iko ligi daraja la kwanza na tarehe 8 mwezi Februari 2014 itacheza na timu ya Mwadui katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga katika mechi ya kwanza raundi ya pili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments