KESI YA PADRI ANAYEDAIWA KUSHINDWA KUTOA MATUNZO KWA MWANAE YAPAMBA MOTO

NB-Siyo picha ya mtoto wa padri Deogratius Makuri
Kesi inayomkabili Padri Deogratius Makuri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida kushindwa kutoa matunzo kwa mwanawe, juzi iliahirishwa tena kwa mara ya tatu baada ya mlalamikiwa kushindwa kufika mahakamani.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini Singida anayesikiliza kesi hiyo, Ferdinand Njau alisema Padri Makuri ametuma mtu aliyedai kuwa ni dada yake kuja kuiarifu Mahakama kuwa hataweza kutokea kutokana na kuumwa.


Hata hivyo, Hakimu Njau alimwambia dada huyo na wasikilizaji kwa ujumla kuwa ili haki itendeke ni lazima mlalamikiwa awepo mahakamani. “Kuna baadhi ya watu wanasema kwa nini labda kesi hii isingesikilizwa faragha eti kisa tunasali naye.
“Hoja kwamba tunasali naye haipo hapa. Ndio maana nimeamua kesi hii isikilizwe Mahakama ya wazi. Nitasimamia kwa nguvu zangu zote nikizingatia sheria hadi haki ipatikane maana nipo kwenye mtego.…. huyu ni kiongozi wangu kanisani, sawa. Lakini pia huyu mtoto, malaika wa Mungu, anahitaji matunzo. Nisipotenda haki, Mungu atanihukumu,” Hakimu Njau alisema. 


  Kutokana na umuhimu huo, Hakimu Njau alisema kuwa endapo mlalamikiwa hatafika tena Januari 3, 2014, ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa, atalazimika kusikiliza kesi hiyo upande mmoja.

Padri Makuri, ambaye pia alikuwa Katibu wa Askofu wakati huo, anatuhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane aliyezaa na Maria Boniphace (26), mkazi wa eneo la Mitunduruni mjini Singida.
Credit-Gumzo la jiji

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post