TAZAMA HAPA KILICHOJIRI KATIKA WARSHA JUU YA ELIMU YA UJASIRIAMALI ILIYOTOLEWA NA WATAALAMU KUTOKA CHUO CHA UALIMU VETA MOROGORO LEO MJINI SHINYANGA KATIKA CHUO CHA VETA SHINYANGA

Awali mwakilishi wa mkuu wa  Chuo cha ualimu cha VETA Morogoro bwana  Anamringi Maro akizungumza katika  warsha juu ya elimu ya ujasiriamali iliyokuwa inatolewa na wataalamu kutoka chuo  cha ualimu Veta Morogoro iliyofanyika katika chuo cha VETA mjini Shinyanga warsha ambayo imekutanisha wakuu na waratibu wa vyuo kutoka vyuo 29 vinavyotoa elimu ya ufundi stadi hapa nchini hususani wakuu wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya magharibi

Aliyesimama ni mkurugenzi  wa VETA kanda ya magharibi inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Tabora,Simiyu na Tabora bi Hildegards Bitegera Bana akitoa hotuba yake leo katika warsha hiyo ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine alitoa shukrani kwa uongozi wa chuo cha ualimu cha VETA Morogoro kwa uamuzi wao wa busara wa kuamua kuleta warsha hiyo muhimu ya elimu ya ujasiriamali awamu ya pili 2010/2014 baada ya awamu ya kwanza 2005/2008 kuisha
Mkurugenzi  wa VETA kanda ya magharibi Bi Hildegards Bitegera Bana akiendelea kutoa hotuba yake kwa wadau hao wa elimu ya ujasiriamali kutoka  vyuo 29 vinavyotoa elimu ya ufundi stadi hapa nchini

Washiriki katika warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika ukumbi wa Chuo cha VETA Shinyanga mjini Shinyanga

Washiriki katika warsha hiyo wakiandika mawili matatu waliyodhani ni muhimu wakati wa warsha hiyo iliyotolewa na wataalamu kutoka chuo cha Ualimu cha VETA Morogoro kwa wakuu wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya magharibi

Mwakilishi wa mkuu wa  Chuo cha ualimu cha VETA Morogoro bwana  Anamringi Maro akielezea kuhusu mradi wa elimu ya ujasiriamali kuanzia awamu ya kwanza 2005/2008 na sasa awamu ya pili 2010/2014 ambapo pamoja na mambo mengine amevitaka vyuo vyote vya ufundi stadi kusimamia elimu ya ujasiriamali ili kuendana na mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa(BIG RESULT NOW).

Mratibu wa mradi wa elimu ya ujasiriamali bwana Lema John akizungumza katika warsha hiyo ambapo amesema kila mtu ana uwezo wa kuwa mjasiriamali ila kinachotakiwa ni kukubali mabadiliko na kujiajiri kunawezekana na kwamba mafanikio ya mjasiriamali hayana mwisho lakini pia akasema ni vyema kwa wale waliofanikiwa kupata elimu hiyo wakawapatia pia watu wengine kwani hapa nchini ziko fursa nyingi na zikitumiwa vizuri umaskini unatoweka

Kushoto aliyesimama ni bwana Yuston mmoja katika ya wajasiriamali waliofanikiwa baada ya kuanza kujishughulisha yeye kaanzisha mradi wa maji katika eneo la Ulyang'hulu akizungumza katika warsha hiyo ya siku moja.Mbali na kuzungumzia mafanikio aliyofikia lakini amesem ni vyema elimu ya ujasiriamali ikapelekwa katika maeneo mengi hapa nchini ili kuwakwamua watanzania kiuchumi.Wa pili kutoka kushoto ni bwana Lema John akionesha kushangazwa na mafanikio ya mjasiriamali Yuston.Waliokaa pembeni pia ni wajasiriamali waliofanikiwa 
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akitoa ushauri kwa wajasiriamali kujenga tabia ya kuweka pesa benki badala ya kukaa nazo majumbani mwao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post