PIKIPIKI YAUA MTOTO KISHAPU


Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la  Jirungu Gerald (4)mkazi wa Kijiji cha Mwandulu kata ya Lagana tarafa ya Negezi wilayani kishapu Mkoani Shinyanga amefariki dunia papo hapo  baada ya kugongwa na pikipiki .

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga ACP Kihenya kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio ambalo limetokea jana majira ya saa kumi na mbili jioni baada ya mwendesha pikipiki kumgonga mtoto huyo na kusababisha kifo chake baada ya kushindwa kumkwepa mtoto huyo.

Amemtaja mwendesha pikipiki huyo kwa ni  Paulo Martine mkazi wa kijiji cha Sanjo wilayani humo aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajiri T,464 CPD aina ya T,BETTER  mali ya Felis mfanyabiashara wa mjini Shinyanga

Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi na kuongeza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la polisi huku akitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani pamoja na wazazi kuchunga watoto wenye umri mdogo wasicheze kandokando ya barabara


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post