Na Valence Robert-Geita
Mwandishi wa
Habari wa Redio Free Afrika Mkoani Geita Bw Salum Maige amelazwa katika
hospitali ya wilaya ya Geita mkoani
Geita baada ya kujeruhiwa vibaya sana
kutokana na kushambuliwa na kundi la Askari polisi wa kituo cha polisi Geita.
Akizungumza
na waandishi wa habari Bw maige ambaye
amelazwa katika chumba NO,4 wodi No 2 katika hospitali ya wilaya hiyo amesema
alishambuliwa jana majira ya saa moja kamili usiku na kundi la askari polisi
zaidi ya watano akiwa umbali wa mita 60 kutoka zilipo ofisi za polisi mkoa
pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa,
Amesema siku
hiyo akiwa anatoka eneo hilo akielekea nyumbani
kwake mtaa wa Bomani alikutana na kundi hilo la
polisI waliokuwa na gari NO,za usajili PT 1998 ocd Geita ambapo baadhi yao walishuka kutoka
kwenye gari na kumueleza kwaMba yuko chini ya ulinzi anaitajika polisi mara
moja,
Ameongeza
kuwa alilazimika kuwauliza polisi kosa lililosababisha ahitajike polisi lakini
badala ya kumjibu walimshika na kufunga pingu mikononi kisha kumtupia ndani ya
gari na kumshambulia kwa kipigo na huku akiwa amekanyagwa kichwani.na askari
awo.
Kufuatia
kipigo hicho Maige amejeruhiwa vibaya
jicho la upande wa kushoto ambapo kwa mujibu wa Daktari aliyemfanyia uchunguzi
kwenye jicho amesema amepasuka mishipa yake kwa ndani kutokana na kipigo hicho hali iliyosababisha damu nyingi kuvuvjia
ndani ya jicho,
“Kwakweli
amepasuka mishipa na hatujui kama itapona lakini tunajitaidi kumpa huduma
lakini nawashangaa awa polisi hawana hata huruma huyu wanamfahamu wamemfanyia
hivi je kama hawakujui si wanakuua kabisa” alisema
dakrai huyo.
Akifafanua zaidi
kuhusiana na tukio hilo Maige amesema katika siku za hivi karibuni amekuwa
katika mgogoro wa kifamilia na mkewe hali iliyosasababisha mkewe kwenda
kumshitaki polisi ambapo polisi waliamua kwenda kumkamata kabla hata ya
kufungua mashitaka na baada ya kufikishwa polisi ndipo alipokuta mkewe na
kuanza kumfungulia mashitaka,
Hata hivyo
katka hali ya kushangaza pamoja na kujeruhiwa vibaya polisi walikataa
kumpatia fomu kwa ajili ya kwenda kupata matibabu hali iliyosababisha kushindwa
kupata matibabu hadi leo asubuhi ambapo baadhi ya waandishi walilazimika kwenda
naye polisi na kudai apatiwe fomu hiyo na kwenda kupatiwa matibabu.
Kwa upande
wake Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina
msaidizi mwandamizi wa polisi Leonard Paul hakupatikana kuzumgumzia tukio hilo la shambulio dhidi
ya mwanahabari huyo lakini kaimu wake Bi Pudensiana Protas
alithibitisha kupewa taarifa juu ya kukamatwa kwa mwndishi huyo lakini
hakujulishwa juu ya kupigwa kwake.
Hata hivyo
baada ya kuoneshwa picha za majeraha ya mwandishi huyo ofisini kwake alionekana
kushutuka na kuahidi kwenda hosptalini kufanya mazungumzo na mwandishi huyo na
kwamba baada ya hapo atafuatilia suala hilo
kabla ya kulitolea maelezo ya kina.
Tukio hilo
limewaachia na maswali mengi baadhi ya wananchi na waandishi wa habari wa mkoa
wa Geita wanaojiuliza je kwa tuhuma za
madai yaliyowasilishwa juu ya mgogolo wa kifamilia kati ya mwandishi huyo na
mkewe ilikuwa sababu ya yeye kutafutwa na askari zaidi ya 5 tena wakiwa na
bunduki gari na kumkamata na kumtia pingu kisha kushambulia kwa kipigo
kama jambazi ama kuna jambo jingine nyuma ya pazia.