Majanga!! KINGWENDU ADAIWA KUMTAPELI MR BONDI LAKI

Kingwendu
Mr Bondi aliskika hivi karibuni akizungumza kwa njia ya simu katika Radio moja hapa jijini Dar esa Salaam akimlaumu Vikali Msanii Mwenzake 

Kingwendu kumtapeli shilingi Laki 2 alizompa kama advance ya Kufanya shooting ya Move yao Mpya ambayo  Wamo Mastaa kibao akiwemo Yeye Mr Bondi,Natasha,Monalisa na Wengine Kibao.


Alichokifanya Kingwendu ni kutoonekana siku ya kufanya hiyo filamu na kuzima simu zake kwa siku sita bila taarifa yeyote na mbaya zaidi alimdanganya Mr Bondi kuwa mama yake anaumwa hivyo anaenda kumwona ila atawahi kurudi kabla ya siku ya shooting.

Taarifa zaidi ni kwamba Kingwendu alipata show nchini Msumbiji.Baada kutafutwa na waandishi wa habari Kingwendu alisema  ni kweli Mr Bondi alimpa laki 2 kama advance na alikuwa Tayari kufanya hiyo kazi ila kwa Bahati nzuri alipata show Msumbiji na waliompa show walimdanganya kuwa wamemkatia tiketi ya ndege ya go and return hivyo alijua angewahi.

Kingwengu alisema mbaya zaidi alipofika kule ikawa shida kurudi baada ya kukosa ndege.Hivyo ilibidi asubiri Ndege.

Hata hivyo amemuomba radhi Mr Bondi kwa kitendo alichokifanya na Anamuomba amsamehe sana yeye ni Binadamu na kilichomponza ni Ndege,alijua angewahi.

Chanzo-babamzazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments