Mauaji tena!!! JAMAA AUAWA KWA KUPIGWA MAWE KISHA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUIBA NG'OMBE KWENYE ZIZI



Mwanamme mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ameuawa kikatili kwa kupigwa mawe na fimbo kisha mwili wake kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba ng’ombe wawili kwenye zizi la mkazi wa kijiji hicho wenye thamani ya shilingi laki 8 katika kijiji cha Mwanima kata ya Sekebugoro wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya alisema tukio hilo limetokea jana saa tisa na nusu mchana baada ya mwanamme huyo ambaye hakuweza kufahamika jina kabila wala makazi yake baada ya kudaiwa kuiba ng’ombe,wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kumshambulia kwa kumpiga fimbo na  mawe kisha kumchoma moto  na kusababisha kifo chake.

 Ni siku chache tu zimepita ambapo  mwanamme mwingine aliyefahamika kwa jina la Majura Mayumba (34) mkazi wa kijiji cha Negezi tarafa ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga aliuawa kwa silaha za jadi baada ya kuiba  ng’ombe  mmoja mwenye thamani ya shilingi laki 5 katika kijiji hicho.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post