TAZAMA TUKIO LA UZINDUZI WA MASHINDANO YA DIWANI CUP KATA YA MJINI SHINYANGA ,MICHEZO AMBAYO IKO CHINI YA DIWANI WA KATA HIYO MHESHIMIWA GULAM HAFIDH ABUBAKAR MUKADAM,AMBAYE PIA NI MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA SHINYANGA

Wa tatu kutoka kulia ni diwani wa kata ya Mjini Shinyanga,ambaye pia ni mstahiki meya Manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafidh Abubakar Mukadam leo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Diwani Cup kata ya Mjini Shinyanga,katika Viwanja vya SHY-COM,mashindano yatakayodumu siku tatu yakijumuisha mitaa mitatu ya Buzuka,Miti mirefu na Kaunda.Hapa anaangalia mechi ya Netiboli kati ya timu ya mtaa wa Buzuka na Miti mirefu

Awali timu ya mtaa Buzuka (jezi nyekundu) na  Miti mirefu (jezi bluu) ambapo katika mpambano huo Miti mirefu wameibuka washindi kwa kuwabamiza goli 17 na  Buzuka wakiambulia goli 9 pekee

Muda mchache baada ya Mechi kati ya Miti mirefu na Buzuka kuisha.picha ya pamoja Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mtaa wa Miti mirefu bi Zainabu Habibu,wa pili ni mratibu wa mashindano ya Diwani Cup bwana Rashid Abdallah,ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Kaunda,wa tatu Diwani Mukadam akifuatiwa na mwenyekiti wa ccm kata ya Mjini Shinyanga bwana Rajab Abbas

Wingu nene likatanda kabla ya mpira wa miguu kuanza kati ya Miti mirefu FC dhidi ya Buzuka FC 

Mwanamichezo,matangazaji RADIO Faraja bwana Isaack wa Eddo akiangalia yaliyokuwa yanajiri katika Viwanja vya SHY-COM,wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Diwani CUP yakisimamiwa na Diwani wa Kata ya Mjini Shinyanga,ambapo fainali itakuwa tarehe 12.12.2013,huku michezo mbalimbali itafanyika siku hiyo kama vile kukimbiza kuku,kuvuta kamba,mbio za magunia n.k.

Mgeni rasmi mwenyekiti wa ccm kata ya Mjini Shinyanga bwana Rajab Abbas akisalimiana na wachezaji wa timu ya Buzuka fc leo wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya diwani CUP 

 Zoezi la ufunguzi linaendelea ambapo mgeni rasmi amesema lengo la mashindano hayo ya siku kuwa ni Burudani zaidi kwa wakazi wa kata hiyo na kwamba siku ya mwisho washindi na washindwa katika mpira wa miguu watapewa zawadi ya laki 1 kila mmoja huku timu za netiboli washindi na washindwa watapewa zawadi ya shilingi elfu 75 na washindi katika timu zote watapewa kombe
Mbele ni mgeni rasmi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Diwani Cup ,yakiwa yamefadhiliwa na diwani wa Kata hiyo(wa pili kutoka kushoto) amabpo amewataka washiriki katika mashindano hayo kupendana,kushirikiana na kujenga mahusiano mazuri na kuongeza kuwa lengo la michezo hiyo ni kuleta fuaraha kwa wakazi wa kata ya Mjini Shinyanga

Diwani wa kata ya Mjini Shinyanga,ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafidh Abubakar Mukadam akizungumza mawili matatu na waandishi wa habari uwanjani hapo ambapo amesema ameamua kuanzaisha mashindano hayo yaliyokuwa yamesimama kwa muda baada ya yeye kuugua na kwenda nchini India kutibiwa.Amesema amenunua jezi yeye mwenyewe kama diwani wa kata hiyo.Lengo la mashindano hayo kuleta furaha na mshikamano kwa wakazi wa kata hiyo.Baada ya mashindano hayo ya Diwani CUP,pia shule za kata hiyo nazo zitafanya mashindano kabla ya mashindano ya manispaa ya Shinyanga kufanyika

Mchezo kati ya timu ya mtaa wa Miti mirefu (jezi za kijani) na Buzuka fc ukiendela kabla ya mvua kuanza kunyesha

Hadi katika dakika za mwisho za mchezo huo mvua ilikuwa inanyesha kama unavyoona uwanja umejaa maji.Hadi dakika 90 zinakamilika Buzuka fc ilipata bao moja huku Miti mirefu wakiambulia 0

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post