Ni balaaa!!! SHUHUDIA HAPA TUKIO ZIMA LA MKUTANO WA MBUNGE WA SHINYANGA MJINI MHESHIMIWA STEPHEN MASELE NA MWIGULU NCHEMBA WA IRAMBA MAGHARIBI ULIVYOFUNIKA JIONI HII MJINI SHINYANGA

Awali viongozi mbalimbali wa CCM muda mchache tu baada ya kuingia eneo la Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo kata ya Kambarage mjini Shinyanga leo jioni.Kulia ni mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri wa madini Mheshimiwa Stephen Masele akiingia kwa kucheza wimbo wa CCM uliokuwa unapigwa katika eneo la mkutano wa hadhara

Mheshimiwa Stephen Masele ,akimkaribisha mheshimiwa Mwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la  Iramba magharibi mkoani Singida iliazungumze na wakazi wa Shinyanga

Mbunge wa Iramba Magharibi  Mwigulu Nchemba,ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa CCM, akizungumza katika mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba wananchi wa Shinyanga kumuunga mkono mbunge wao Stephen Masele kwani mbunge huyo kijana anayajua vyema matatizo ya watu Shinyanga.Lakini pia aliwataka watanzania kuondokana na ugeni wa siasa ya vyama vingi hivyo kupendana na kushirikiana na viongozi wao katika kuleta maendeleo katika jamii hasa baada ya uchaguzi

Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia hotuba ya Mheshimiwa Nchemba katika eneo la mkutano

Kushoto ni mheshimiwa Masele  akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na wananchi  wakifuatilia hotuba ya mheshimiwa Nchemba

Ndivyo hali ilivyokuwa baadhi ya wananchi walikuwa mbali kidogo na eneo la mkuatno lakini wanafuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo

Mkutano unaendelea

Mheshimiwa Nchemba akimtambulisha  kijana aliyejulikana kwa jina la Musa Tesha mkazi wa Tabora(Kushoto) anayedaiwa kumwagiwa tindikali na vijana wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA huko Tabora na kusababisha kuharibika kwa sura yake.Akizungumza katika mkutano huo kijana huyo amesema alitekwa na vijana wa CHADEMA,akapigwa,kuteswa na kumwagiwa tindikali ,akapelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu na kuwashauri wananchi wa Shinyanga kukiepuka chama hicho.

 Wananchi wakisikiliza maelezo ya kijana anayedaiwa kumwagiwa tindikali,ambapo kijana huyo alisema mmoja wa wahusika wa tukio hilo yumo pia kijana mkazi wa Shinyanga
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa Stephen Masele upande wa kushoto jukwaani akizungumza katika eneo la mkutano ambapo aliwaomba viongozi mbalimbali katika jimbo lake kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zahanati,vyoo vya shule,masoko n.k.Hata hivyo alieleza kukerwa na baadhi ya madiwani katika jimbo lake hasa kutoka vyama vya upinzani wanaokwamisha miradi ya maendeleo mfano kata ya Masekelo,Ndala na Kitangiri.

Mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo wakiwa eneo la mkutano



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments