Huan Chuncai mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa jimbo la Hunan anasumbuliwa na tatizo la nyama kukua kwa kasi katika kichwa chake hususan maeneo ya uso.Picha hapa chini zinaonesha akifanyiwa oparesheni |
Bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Huan Chuncai mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa jimbo la Hunan anasumbuliwa na tatizo la nyama kukua kwa kasi katika kichwa chake hususan maeneo ya uso,ugonjwa ambao umetambulika kama neurofibromatosis ambao husababishwa na ukuaji wa cell ambalo ni moja ya matatizo ya kijetiksia. kwa mujibu wa the dailymail kijana huyo amesumbuliwa na tatizo hilo toka angali mdogo akiwa na umri wa miaka minne.
Tayari amekwisha fanyiwa opesheni mara mbili kabla katika miaka tofauti tofauti (yaani mwaka 2007 na mwka 2008).
Huan amepoteza meno yake yote akiwa na umri wa miaka 25 hali inayompelekea apate shida kwenye kuongea pamoja na kula.
Kijana huyo ambaye amekuwa akiitwa 'China's Elephant Man amekuwa akiishi kwa shida sana,kwa miaka mitano iliyopita nyama hizo zilikuwa na uzito wa 33lb (15kg) na kumsababishia matatizo ya uti wa mgongo kupelekea maumivu makali anayoyapata kutokana na kuongezeka kwa nyama hizo.
Huan amefanyiwa opesheni tena kuondoa nyama hizo kwa sasa zilizokuwa na uzito wa 3.3lb (1.5kg).
Opesheni yake huwa ni ya hatari sana kwani hupelekea kuvuja kwa damu nyingi sana mwili mwake.
Credit-This day magazine
Post a Comment