Ukatili!!! MFUGA NGURUWE ABAKA MTOTO WA MIAKA 6 KWA PIPI

Mtoto mmoja, mkazi wa Kitunda (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 6 amebakwa na mfanyakazi wa kufuga nguruwe aishie maeneo ya jirani baada ya kumrubuni binti huyo mwenye umri wa miaka 6 kuwa atamnunulia pipi.


Akizungumza kwa uchungu, baba wa mtoto huyo, Joseph Isaac alisema mwanaye alibakwa na mfanyakazi huyo wa nguruwe aliyemtaja kwa jina la Fabiano baada ya kumuahidi kuwa atampa pipi.



“Siku hiyo nilirudi nyumbani nikamkuta mwanangu anachemka homa kali, nikamwambia mama yake amuogeshe tumpeleke hospitali kwani tulikuwa tumeshampatia dawa ya kutuliza lakini haikumsaidia,” alisema baba huyo.



Mama wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Elizabeth, alimuogesha mwanaye na kugundua kuwa alikuwa amevimba sehemu za siri kutokana na majeraha aliyopata na alipombana ndipo alipomtaja mfanyakazi huyo wa nguruwe.



“Nilimwambia mume wangu tukachukue PF3 (fomu ya uthibitisho wa polisi) kisha tukatibiwe. Tulienda Kituo cha Polisi Stakishari na  kuandikisha RB No KIT\RB\2804\2013 KUBAKA ndipo tukaenda Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu,” alisema mama huyo.



Walipofika katika Hospitali ya Amana, walilazimika kulazwa kwa siku tatu kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa nayo mtoto huyo wakati huohuo polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa (Fabiano).



Ilielezwa kuwa, pamoja na mtuhumiwa kukamatwa lakini alitolewa kwa dhamana hivyo wazazi wa mtoto huyo kuhoji kulikoni aachiwe.



Waandishi wa habri walikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Anna Kosmas ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuambatana na waandishi hadi nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo walielezwa kuwa ametoweka.



Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi aliahidi kufuatilia suala hilo kwani limesharipotiwa kituoni hapo na atahakikisha mtuhumiwa anakamatwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments