![]() |
NB-Picha haiendani na habari hapa chini |
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa
Kijiji cha Majalila wilaya ya Mpanda mkoani Katavi ameuawa kwa kupigwa na fimbo
kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake wa kambo
aitwaye Hamisi Mohamed.
Tukio hilo
lilitokea hapo juzi majira ya usiku wakati moto huyo alipokuwa
amelala kitandani na wazazi wake.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri
Kidavashari alisema marehemu huyo alikufa baada ya baba yake wa kambo kukasirishwa
na kitendo cha mtoto huyo kulia wakati akiwa amelala kitendo ambacho aliona
kinamnyima usingizi.
Alisema kitendo hicho cha mtoto kulia kilimfanya baba
huyo wa kambo kimkasirishe na ndipo alipoanza kumpiga fimbo sehemu mbalimbali
za mwili wake huku mama wa motto akimsihi baba huyo wa kambo aache kumpiga
mtoto huyo.
Alieleza baada ya kuona hali ya motto huyo imekuwa mbaya baba huyo wa kambo alimuaga
mkewe kuwa anakwenda dukani kumnunulia dawa za maumivu.
Baada ya baba huyo wa kambo kwenda dukani mtoto huyo alifariki
ikiwa ni muda mfupi tu toka baba yake
huyo wa kambo alivyokuwa amekwenda dukani ambapo alitokomea kusiko julikana.
Kamanda Kidavashari alisema uchunguzi wa awali wa baba
wa kambo kumuua mtoto huyo ni chuki baina ya mama wa mtoto huyo aitwaye
Diana Philipo na mume wake ambaye hakutaka marehemu aishi nyumbani
kwake.
Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili
likimkamata limfikishe kwenye vyombo vya sheria .
Na Walter Mguluchuma.
Post a Comment