Ndivyo ilivyo!! TAZAMA HALI HALISI YA MAZINGIRA KATIKA BAADHI YA MAENEO MJINI SHINYANGA

Haya sio maji yanayotokana na mvua bali ni maji yanayotoka katika bomba la maji,haijulikani ni kwanini yanavuja na yanavujia wapi,lakini ukifika katika eneo la Bimbo maarufu kwa mzee Msenda kata ya Ndembezi ndani ya Manispaa ya Shinyanga utajionea maji yakivuja katika barabara,haijulikani kama mamlaka ya maji safi na maji taka katika manispaa ya Shinyanga SHUWASA inatambua kuwa katika baadhi ya maeneo mabomba ya maji yamepasuka au kuharibika

Ni katika eneo la barabara inayotoka Bimbo hadi OXFAM,zaidi ya miezi mitano maji yamekuwa yakivuja na kufanya barabara hiyo iwe kero kwa wapitaji na pengine wakazi wa eneo hilo kukumbwa na wimbi la mbu


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post