RAGE NOMAAA!!! AGOMA KUITISHA MKUTANO WA DHARURA NA WANACHAMA KAMA ILIVYOAGIZWA NA RAIS WA TFF

Hatimaye mkutano wa Mwenyekiti aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage na waandishi wa habari umefanyika leo mchana kama alivyohaidi jana.

Katika mkutano huo Rage amegoma kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama kama alivyoagizwa na Rais wa shirikisho la soka nchini Bwana Jamal Maliniz mapema jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Rage amesema kwamba haoni sababu za kuitisha mkutano mkuu na endapo TFF na Malinzi wataendelea kumshinikiza kufanya hivyo basi atajiuzulu.

Katika hatua nyingine Rage amemteua mwanachama wa klabu hiyo Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba.

Pia, amemteua Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post