MWIZI MWINGINE AUAWA SHINYANGA ,NI BAADA YA KUVAMIA NA KUIBA NG'OMBE WILAYANI KISHAPU


NB siyo Ng'ombe aliyeibiwa

Wanakijiji wa  kijiji cha Negezi tarafa ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamemuua kwa kumpiga mawe na marungu Majura Mayumba (34) na kusababisha kifo chake papo hapo baada ya  kuiba  ng’ombe

Walioshuhudia tukio hilo wamesema kijana huyo ameuawa  jana majira ya saa tatu usiku baada ya  kuvamia nyumbani kwa Shija Kazara na kuiba ng’ombe (maksai).

Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache tu baada ya kijana mmoja mjini Shinyanga kuuawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kuiba na kumchoma kisu mwendesha baiskeli,

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post