Hatari !!! MWANAMME AKUTWA AMEKUFA NDANI YA MTO KATIKA DARAJA LA IBINZAMATA MJINI SHINYANGA

Mwili wa marehemu (haupo) umekutwa ndani ya mto Kidaru katika daraja la  Ibinzamata mjini Shinyanga.ulikuwa mbele ya mawe hayo mawili unayoyaona ndani ya maji

Wakazi wa eneo hilo wakiangalia eneo alimofia marehemu mara baada ya mwili wa marehemu kuchukuliwa na polisi 

Ikiwa ni siku mbili tu baada ya mwanamme mmoja huko wilayani Kishapu kukutwa amekufa ndani ya mtaro kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ulevi ,hapa mjini Shinyanga leo Sabas Jumanne Mlengela(54)mkazi wa kitongoji cha Bugwandege kata ya Ibinzamata mjini Shinyanga amekutwa amekufa kwenye mto wa daraja la Kidaru maarufu Daraja la Ibinzamata huku akiwa na baiskeli yake ndani ya maji huku hofu ikitanda kwa wakazi wa eneo hilo kuwa huenda kifo chake kinatokana na kuuawa kisha kutumbukizwa katika mto huo

Tukio hilo limetokea leo saa moja asubuhi  ambapo Sabas Jumanne Mlengela,ambaye ni mkaguzi wa hesabu katika shirika la COASCO Shinyanga alikutwa amekufa maji kwenye mto wa daraja hilo mwili wake ukiwa unaelea juu ya maji.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulikutwa umezama kwenye mto huo pamoja na baiskeli yake na simu yake na kalamu vilikuwa vimeanguka pembeni mwa mto huo na mwili wake ukiwa hauna majeraha yoyote.

Kamanda Kihenya asema kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa ndugu zake na marehemu walisema jana majira ya saa tatu usiku walikuwa na marehemu kwenye kikao cha kuvunja kamati katika bar iitwayo Baelezee na marehemu aliondoka kurudi nyumbani na hakuonekana tena hadi alipogundulika akiwa amekufa leo asubuhi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post