|
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe ulioachwa na marehemu huyu |
Barua aliyoacha marehemu |
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma shule
ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa
kurudia kufanya mtihani wa taifa wa kidato
cha nne kupitia kituo cha Krelluu mjini Iringa Khamis
Mkundo mkazi wa Mwangata C katika manispaa ya Iringa
amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile alichodai kuchoshwa
na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndefu
aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si
kwa kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa
mara hivyo kuamua kujiua ili kuepuka na aibu katika
mtihani ujao ambao anaamini angefeli.
Shemeji wa kijana huyo Aden Tagalile
amesema kuwa
tukio hilo limetokea jana mida ya kati ya saa 12 na saa 1 usiku
wa leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda mrefu kwa
kijana huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi
mtihani wa kidato cha nne bila mafanikio.
Kwani alisema hajapenda kuona anaendelea
kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo
mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo
aliangana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi nae kwa kila mmoja
kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa
amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Sarehe
Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe
ambao kijana huyo ameuacha .
CHANZO: Tuangaze
CHANZO: Tuangaze
Post a Comment