Akiwa na umri wa miaka 58 Muhindi mmoja anayekwenda
kwa jina la Ram Singh Chauhan anajivunia kuwa mtu mwenye mustachi mrefu kuliko
wote duniani, ukiwa na urefu wa fyti 14.
Chauhan, ambaye alikua na kuishi kwenye jiji la
Jaipur ndani ya jimbo la Rajasthan, mustachi huo ni fahari yake kuu. Ametumia
miaka 32 kuufuga na kuupa matunzo yaliyoweza kuupelekea kufika hapo.