MAUAJI TENA KAHAMA -MWANAMKE AVAMIWA AKIWA AMELALA KISHA KUKATWA PANGA NA UTUMBO KUTOKA NJE



Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Nkwimba Sahani (55) mkazi kijiji cha  Nhandu kata ya Chela tarafa ya Msalala  wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kikatili baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwa kumkata mapanga shingoni na tumboni na kupelekea utumbo wake kutoka nje na kufa papo hapo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amesema  hilo limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba usiku  ambapo  watu hao baada ya kuvunja mlango na walianza kumshambulia kwa kumkata  panga shingoni,mkono wa kushoto na tumboni na kusababisha utumbo wake utoke nje na akafariki dunia .

 Amesema  wakati tukio hilolinatokea mwanamke huyo alikuwa amelala nyumbani kwake ndipo  ghafla akavamiwa na watu wasiojulikana na kumshambulia hatimaye kumsababishia kifo.
Amesema Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post