NB-Siyo picha ya Mwami Mwanalusi |
Mtu mmoja Mkazi
wa Kijiji cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Mwami Mwanalusi (31)
amekatwa na kisu katika sehemu zake za siri na watu wasiojulikana wakati akiwa amelala
ndani ya nyumba ya shemeji yake na watu wasiojulikana.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo
jana majira ya saa nane usiku nyumbani kwa shemeji yake.
Alisema siku ya
tukio Mwami alikuwa amekwenda kumtembelea shemeji yake
aitwaye Anset Kapampala (36) ambae alikuwa akiishi katika kijiji
hicho cha Majimoto.
Baada ya mlo wa
usiku mwenyeji wake alimwonesha chumba cha kulala ambacho hata hivyo hakikuwa
na godoro wala kitanda bali kulikuwa na Benchi la kupumzikia ambalo shemeji
yake ambae ni mwenyeji wake alimweleza Benchi hilo ndilo alitumie kama kitanda
cha kulalia kutokana na hali yake ya kiuchumi kutokuwa nzuri.
Alisema wakati
Mwami yuko ndani ghafla walitokea watu asiowafahamu ambao waliingia ndani ya
chumba hicho na wala hawakumsemesha chochote hali ambayo ilimfanya
ashikwe na butwaa.
Alieleza ndipo
watu hao walipoanza kumkata kwa kisu sehemu zake za uume hadi uume wake ukawa
umeharibika vibaya na kisha watu hao wakatokomea kusikojulikana na
kumfaya yeye apige mayowe ambapo shemeji yake ambae alikuwa amelala
kwenye nyumba yake nyingine alishtuka na ndipo alipoingia ndani na
kumkuta mgeni wake akiwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri.
Kamanda
Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijulikana na
polisi wanaendelea na upelelezi ili kuwabaini na kuwakamata waliohusika
ili sheria ichukuwe mkondo wake.
Chanzo-katavi
yetu