Siku chache tu baada
ya mwanamme aitwaye Mwami Mwanalusi (31) kukatwa sehemu zake za siri akiwa
amelala nyumbani kwa shemeji yake mkoani Katavi , hali imeendelea kuwa mbaya
ambapo juzi,mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mele Seni
(60) Mkazi wa Kijiji cha Kapalala Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Mkoa wa Katavi ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani na mgongoni na
watu wasio fahamika wakati akiwa nyumbani kwake akiota moto.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo
la mauaji ya kinyama limetokea juzi majira ya saa moja na nusu usiku
nyumbani kwa marehemu huyo kijijini hapo.
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu akiwa
nyumbani kwake amejipumzisha akiota moto ghafla walitokea watu
wasiofahamika na kupiga hodi nyumbani kwa marehemu ambae nae aliwakaribisha
watu hao kwa kujua ni watu wema.
Alieleza ndipo watu hao walipoanza
kumshambulia marehemu kwa kumkata kwa panga kwenye kichwa na mgongoni huku
marehemu akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zake.
Kidavashari alisema licha ya marehemu
kupiga moyowe majirani zake hawakuweza kujitokeza mapema kuweza
kumpatia msaada na ndipo watu hao walipoona Mele Seni amefariki
dunia huku wauaji wakitokomea kusiko julikana.
Majirani waliweza kufika nyumbani kwa
marehemu baada ya muda mrefu wa kutokea kwa tukio hilo ambapo walimkuta
marehemu akiwa ameisha fariki dunia huku mwili wake ukiwa na majeraha ya panga
kichwani na mgongoni na kisha walitowa taarifa kwa uongozi wa serikali ya
kijiji ambao nao walitowa taarifa kwa jeshi la polisi.
Kamanda Kidavashari alieleza kabla ya
tukio hilo marehemu alikuwa akilalamikiwa na majirani
zake na wanakijiji hicho kuwa amekuwa akijihusisha na vitendo vya
kishirikina kwa kuwaroga watu kijijini hapo.
Hivyo uchunguzi wa awali uliofanywa
na jeshi la Polisi umebaini kifo hicho kametokana na imani ya
ushirikina ulisababisha wanakijiji hicho kumjengea chuki marehemu
huyo.
Mpaka sasa hakuna mtu au
watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hili na jeshi la
polisi linaendelea na upelelezi ili kuwakamata na
kuwafikisha mahakamani waliohusika katika tukio hili.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Katavi ametowa wito kwa wananchi kutojichukilia
sheria mkononi kutokana na kuwahusisha watu na imani za
kishirikina na matokeo yake wamekuwa wakiua watu pasipo sababu
N a Walter Mguluchuma
Post a Comment