Wakati Serikali ikisisitiza kuwa huduma ya kumwongezea
mgonjwa damu hospitalini ni bure, imebainika kwamba baadhi ya watu mitaani
wakiwamo wabeba mizigo sokoni wanauza damu zao kwa watu wanaohitaji.
Mbali ya watu kuuza damu zao, majimaji hayo
mekundu muhimu mwilini yamegeuka bidhaa adimu baada ya baadhi ya wauguzi na
madaktari nao kugeuza huduma hiyo kuwa kitega uchumi chao.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ni kosa kwa
mtumishi yeyote wa afya nchini kumuuzia mgonjwa damu na wala hakuna biashara ya
kuuza damu kwa kuwa hutolewa bure na watu wanachangia kwa hiari.
Uchunguzi wa kina uliofanywa katika hospitali mbalimbali
nchini, umebaini hospitali nyingi hazina damu za kutosha na hivyo kusababisha
baadhi ya wagonjwa kuwalipa watu mitaani, ili kuwatolea damu au kuinunua kwa
wauguzi na madakari.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif
Rashid alisema kuwa wahudumu wa afya wanaoendesha vitendo hivyo ni watu
wanaojaribu kuizidi maarifa Serikali na kwamba wananchi wamepewa taarifa za
kutosha kuwa damu haiuzwi.
“Kuna watu wanajaribu kutuzidi maarifa, hiyo ni tabia
inayopaswa kupigwa vita. Mtu yeyote atakayetakiwa kununua damu, atoe taarifa
kwa mganga mkuu au kituo chochote cha polisi,” alisema.
Mkoani Dodoma
Wabeba mizigo wa soko la Majengo Mjini Dodoma, wamekuwa
mkombozi kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali ya mkoa huo baada ya kugeuza
miili yao kuwa
sehemu ya kuvuna damu na kuiuza kwa ndugu wa wagonjwa hao.
Gharama za kuuza damu hiyo ni kati ya Sh10,000 hadi Sh30,000
kwa chupa moja, kutegemea na uwezo wa ndugu wa mgonjwa huyo, lakini baadhi
wamekuwa wakitoa zaidi kama sehemu ya
shukurani.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la mwanachi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuthibitishwa
na baadhi ya wabeba mizigo hao, imebainika kuwa kitendo cha kutoa damu kwa
wabeba mizigo ni cha kawaida na kwamba utaratibu huo ulianza muda mrefu.
Enock Ayub ambaye ni mmoja wa watu ambao wamechangia damu
zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti, alilimbia gazeti hili kuwa biashara ya
kutoa damu anaipenda na kwamba inampa matumaini ya kuishi kwa kuamini kuwa bado
ni mzima.
“Mimi nimechangia damu zaidi ya mara tatu, lakini tukifika
kule tunabadilisha majina maana madaktari wanataka mtu ukae muda za miezi sita
bila ya kutoa, sisi tunataka fedha ‘mkwanja’, hatuna jinsi,” alisema Ayubu na
kuongeza:
Chanzo-mwananchi
Post a Comment