HII NDIYO CHEMICHEMI YA AJABU INAYOTOA MAJI YA MOTO ENEO LA UZOGORE KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA


Hii ndiyo chemichemi inayotoa maji ya moto katika kitongoji cha Uzogore,kijiji cha Ikulilo kata ya Ibadakuli ndani ya manispaa shinyanga ,chemichemi ambayo ilitokea kimiujiza zaidi ya miaka 100 iliyopita

Bwana Omari mkazi wa manispaa ya Shinyanga akiangalia maji yanayotoka katika chemichemi hiyo,ambapo maji hayo yanatumiwa na wakazi wa eneo hilo kwa kuoga na kufualia nguo kutokana na kwamba maji hayo yana radha ya chumvi
Kulia ni mwandishi wa habari gazeti la Habarileo Kareny Masasy akizungumza na bi Nyerobi ambaye ni mmoja kati ya waliosimulia historia ya chemichemi hiyo ambayo inajulikana kwa jina la Chemichemi ya Malembela.Malembela alikuwa mtemi wa Uzogore ambapo baada ya kifo chake chemichemi ya ajabu ilijitokeza eneo la Ndembezi mjini Shinyanga alikozikwa na katika hali ya kushangaza chemichemi hiyo ikahamia eneo la kitongoji cha Uzogore kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post