 |
Waumini pamoja na watu wenye mapenzi mema wakiwemo viongozi
wa serikali,vyama vya siasa waliohudhuria shereheza maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa dayosisi ya Shinyanga kwa kanisa la AICT,sherehe hizo pia zilienda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari maarufu kwa jina la Bishop Nkola
|
 |
Masanja Mkandamizaji akitoa burudani na wacheza shoo wake
|
 |
Waumini wakifuatilia burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali
wa nyimbo za injili kama vile AIC
Shinyanga,AIC Kambarage,AKC kwaya,Masanja Mkandamizaji pamoja na CVC Chang’ombe
vijana kwaya kutoka jijini Dar es salaam
|
 |
Chang’ombe vijana kwaya wanafanya mambo ndani ya uwanja wa
kambarage mjini Shinyanga
|
 |
Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Sengerema
mheshimiwa Willium Ngeleja akizungumza uwanjani hapo ambapo aliwataka wananchi
kuepuka manabii wa uongo ili kuhakikisha kuwa amani ya nchi inaendelea kuwepo |
 |
Askofu mkuu wa kanisa la AICT dayosisi ya Shinyanga Dk John
Kanoni Nkola akihubiri katika kilele cha maadhimisho ya miaka ya 20 tangu
kuanzishwa kwa kanisa hilo,maadhimisho hayo yamefanyika jana katika uwanja wa
CCM Kambarage mjini Shinyanga,ambapo pia kulifanyika harambee ya ujenzi wa
shule ya sekondari ya Bishop Nkola inayomilikiwa na kanisa hilo
|
 |
Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Anna Rose
Nyamubi akiwa na (Prince Mobutu)na mtoto wa Mobutu Seseseko ambaye pia
alihudhuria maadhimisho hayo na kuchangia Euro 2000 pamoja na makontena
mawili,moja la nondo jingine la saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Bishop
Nkola.Mkuu wa wilaya aliuambia umati wa watu waliohudhuria kuwa shule ya Bishop
Nkola ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri mkoani Shinyanga. |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment