JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI

Na Valence Robert, Geita

Jeshi la polisi mkoani Geita limetakiwa kufanya kazi kwa kushirkiana na wananchi ili wananchi waweze kuwapatia askari taarifa za wahalifu.

 kauli hiyo imetolewa leo na naibu kamishina wa polis Sospeter kondela wakati wa kuzindua bwalo la polisi la mkoa wa Geita katika makao makuu ya mkoa wa Geita,

Amesema askari polisi wanatakiwa kushirikiana na wananchi ili kupata taarifa za wahalifu na sio kuwatisha wananchi.

Aidha amesema  kuna baadhi ya polisi  wamekuwa wakiwatishia wananchi na kuwabambikizia  kesi ambapo amesema kama watabinika  watachukuliwa hatua kali.

Pamoja na mambo mengine  amefungua bwalo la polisi na kutoa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na mgodi wa dhahabu  [GGM ] pamoja na wadau mbalimbali kama vile vitanda vyoo na mahema vyote vikiwa na thamani ya shlinga milioni mia mbili themanini na sita.

Naye kamanda wa jeshi la poli mkoa wa Geita Leonard Paulo aliwashukuru wadau pamoja na mgodi huo [GGM] kwa msaada walioutoa na kwamba wananchi wa mkoa wa Geita kwa kuendelea kutoa ushirikiano  na mzuri na kuwafichua askari wanaowasunbua.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mgodi wa [GGM] Bw Michael Van alisema wameamua kutoa misaada hiyo kwasababu ya ushirikiano uliopo kati ya polisi na mgodi na kuahidi kuendelea kulisaidia jeshi hilo na wasisite kuomba msaada pale wanapohitaji,

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post