SHUHUDIA TUKIO ZIMA LA MKUTANO WA CHADEMA MJINI SHINYANGA,UKIONGOZWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MASWA MASHARIKI SYLVESTER MHOJA KASULUMBAYI

Awali afisa wa Chadema kanda ya ziwa mashariki bwana Frank Kubwera akiwasalimu makamanda wa Chadema waliohudhuria mkutano wa hadhara katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa shinyanga kuendelea kukiunga mkono chama chake huku akiwapongeza wananchi hao kwa kumpa kura aliyekuwa mgombea wa jimbo la shinyanga mjini mwaka 2010 marehemu Philip Shelembi,ambapo katika uchaguzi huo Steven Masele wa CCM alitangazwa mshindi katika uchaguzi

Mwanyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga bwana Juma Protas akizungumza mjini shinyanga kabla ya mgeni rasmi mheshimiwa Kasulumbayi hajaanza kuwahutubia wananchi.Protas aliwaomba wakazi wa jimbo la Shinyanga mjini kukiunga mkono  chama hicho katika mchakato wanaotarajia kuufanya kuanzia Novemba 4 mwaka huu  wa kupita mtaa kwa mtaa,kata kwa kata katika jimbo la Shinyanga mjini kumshtaki mbunge wa jimbo hilo Steven Masele wa CCM kwa wananchi kwa kuwatukana  wananchi hususani vijana hivi karibuni kwamba VIJANA WANATUMIKA KAMA KONDOMU katika kudai haki ambapo wananchi wataamua kama mbunge huyo alikuwa sahihi kusema hivyo.Mbali na hilo bwana Protas alisema hivi sasa CCM imezeeka ndio maana wanakodi Wachina ili wawe vivutio kwenye mikutano yao kama ilivyofanyika hivi karibuni mkoani Shinyanga wakati wa ziara ya katibu mkuu wa ccm taifa ndugu Abdulrahman Kinana.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakiinyoosha mikono baada ya kuulizwa na viongozi wa CHADEMA kama wanaunga mkono harakati za chama hicho

Mambo ndivo ilivyokuwa  hata waendesha baiskeli maarufu kwa jina la daladala wanoutumia muda mwingi kusafirisha abiria nao walikuwepo kusikiliza sera za Chadema kwa kuamini kuwa chama hicho ndiyo mkombozi wao

Mkutano  wa hadhara unaendelea wananchi wanatafakari

Makamanda wa Chadema wakitafakari hotuba ya mbunge wa jimbo la Maswa mashariki lililopo mkoani Simiyu Sylvester Kasulumbayi

Mkutano unaendelea

Wengine walidiriki kukaa kwenye kivuli cha nyumba iliyokaribu na uwanja wa mkutano kufuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano wa hadhara

Mbunge wa jimbo la Maswa mashariki Sylvester Mhoja Kasulumbayi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema serikali ya CCM inakumbatia ubaguzi mfano katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro mifungo ya wafugaji wa Kabila la wasukuma ikisogea eneo hilo mifugo inakamatwa huku wafugaji wa kabila la wamasai wakiruhusiwa kufuga ndani ya eneo hilo bila kukamatwa na mpaka sasa zaidi ya ng'ombe elfu 12 wamekamatwa na kushikiliwa.Akaongeza kuwa ni wakati mzuri sasa watanzania kubadilika na wasukuma kuamka kwani maisha yao yako chini pamoja na kuwepo kwa madini ya dhahabu na almasi huku akisema kuwa Chadema hawaogopi kupigwa mabomu hivyo harakati zitaendelea kwani kama ni kufa kila mwanadamu lazima atakufa na kwamba mtu anayekufa akipigania haki daima atakumbukwa

Gari la matangazo la Chadema linatumika kwa ajili ya sauti kuwafikia wananchi baada ya TANESCO kukata umeme wakati Mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki Sylvester Mhoja Kasulumbayi akihutubia wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kukiunga mkono chama hicho na kuongeza kuwa vijana ndiyo watakaoleta mabadiliko hapa nchini kwani Chadema ni wasema kweli huku akisema kuwa kama serikali haitabadilika basi CHADEMA itailazimisha kubadilika
Mapema kabisa wakati mkutano unaanza mwanaharakati wa CHADEMA bwana Francis Kasili akiwasalimu wakazi wa Shinyanga ambapo alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na wananchi pamoja na kwamba CCM wanatumia pesa na kumfanya mtanzania aonekane hafai

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment