Imebainishwa kuwa katika kipindi cha mwezi Januari
hadi mwezi Agosti mwaka huu ajali za barabarani katika mkoa wa shinyanga zimepungua
kwa asilimia 12.6 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo ilikuwa
asilimia 33.7
Hayo yamebainishwa juzi na
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga RTO Desdery
Kamugisha wakati akitoa
takwimu hizo kwa waandishi wa habarii, ambapo alisema katika kipindi cha mwezi
januari hadi Agosti mwaka zilitokea ajali 167 kati ya ajali hizo
zilizosababisha vifo ni 65 ,majeruhi 102 ambapo jumla ya watu waliokufa
ni 84 na waliojeruhiwa ni 191.
Aidha alisema ajali
nyingi mkoani Shinyanga zinatokana na uzembe wa madereva, ulevi pamoja na
waendesha baiskeli maarufu daladala na pikipiki wengi wao wakitokea maeneo ya
vijijini wanaofanya shughuli hizo mjini Shinyanga wengi wakiwa hawajui
sheria na alama za usalama barabarani.
Mwaka jana katika
kipindi kama hicho zilitokea Ajali 191
kati ya ajali hizo zilizosababisha vifo 98,na ajali zilizo sababisha majeruhi
ni 93, na watu waliokufa ni 75, waliojeruhiwa ni 201.