MWANDISHI ANUSURIKA KUPIGWA NA MFANYABIASHARA ALIYEJIGAMBA KUWA JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LIKO MIKONONI MWAKE


Mwandishi wa habari wa gazeti la Mzawa wilayani Geita,Alphonce Kabilondo amenusurika kupigwa na mfanyabiashara wa dhahabu mbele ya kituo cha polisi cha Katoro wilayani hapa wakati akiwa katika majukumu yake ya kazi baada ya kutokea ajali iliyohusisha gari la mfanyabaishara huyo.

Habari zilizoufikia mtandao huu wa www.malunde1.blogspot.com kutoka kwa mkoani Geita zinasema kuwa Kabilondo alikumbana dhahama hiyo majira ya saa 8 mchana alipokuwa akifuatilia tukio la ajali ya barabarani iliyotokea juzi na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo mwendesha bodaboda.

Mfanyabishara huyo anayefahamika kwa jina moja la Obole akiwa katika kituo hicho cha polisi baada ya kugundua kuna waandishi wa habari na ndipo alitoka ndani na kumfuata mwandishi huyo kwa lengo la kumpiga lakini alijihamu kwa kumkwepa.

Hata hivyo aliwazuia waandishi wa habari kulipiga picha gari lake lenye namba za usajili T 910 BSN lililosababisha ajali hiyo baada ya kugongana na pikipiki namba T 579 BUV iliyokuwa ikiendeshwa na Athuman Mrisho(29) akiwa amembeba abiria Dotto Paulo(30)ambao wote walifariki papo hapo.

Aidha katika hali isiyotarajiwa mfanyabiashara huyo alidai kumshughulikia mwandishi yeyote atayeandika habari kuhusiana na ajali hiyo kwa madai kwamba polisi mkoani hapa akiwemo kamanda wa polisi Leonard Paulo liko mikononi mwake.

‘’Kaandike utaona,nitakushughulikia vibaya sana.hunifanyi kitu polisi wote hapa hawanifanyi kitu hata kamanda nafahamiana naye,dhubutu uone’’alisikika Mfanyabiashara huyo.

Kiburi hicho kinatokana na mfanyabiashara huyo mwaja jana kutoa msaada wa kulikarabari gari la polisi la kituo hicho na kwamba mwandihsi huyo alipokuwa akitishiwa kupigwa hakuna polisi aliyejitokeza kumsaidia.

Ajali hiyo imetokea Jana majira ya saa 6 mchana eneo la Kasesa barabara itokayo Katoro wilayani Geita kwenda Rulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Paulo alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia madai ya mfanyabaisha huyo kuliweka jeshi la polisi mikononi mwake,simu yake iliita bila kupokelewa,Ingawa jeshi la polisi wilaya ya Geita limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post