INATISHA!! MWANAMKE AUAWA KIKATILI WAKATI AKITOKA KUJISADIA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawatafuta watu waliohusika na mauaji ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Misoji Kasubi (50) mkazi wa kijiji cha Manhigana kata ya Solwa tarafa ya Nindo, wilaya ya Shinyanga vijijini  ambaye ameuawa kikatili kwa kukatwa  panga kichwani,mdomoni na bega la kushoto wakati akitoka kujisaidia nje ya nyumba yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa saba na nusu usiku na mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana na uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments