|
Aliyesimama ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa
wa Shinyanga (SPC),bwana Shija Felician akizungumza leo wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa
klabu hiyo ambao umefanyika katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel mjini
Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alikemea vikali tabia ya baadhi ya wanachama wake kukiuka maadili ya kazi ambapo baadhi yao wanatumia lugha chafu na kuendekeza pesa badala ya kazi na kusababisha kero katika jamii |
|
Mkutano unaendelea |
|
Mweka hazina wa SPC bi Stella Ibengwe akisoma taarifa kuhusu mapato na matumizi
ya klabu hiyo kwa mwaka 2013 |
|
Picha ya pamoja ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambapo sasa wamefikia 32 baada ya
mkutano huo mkuu wa mwaka kumepokea majina ya wanachama wapya
9 walioomba uanachama ambao tayari kikao cha kamati tendaji kilikuwa
kimewapitisha nao ni Bi Lucy Masalu,Paulo Kayanda,Happiness
Kihampa,Herieth Katikiro,Neema Mghen,Shangwe Than,Geni Elius na Michael Maduhu na bwana Kadama Malunde ambaye ndiyo mkurugenzi wa blog hii ya malunde1.blogspot.com.
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553