UKATILI WA KUTISHA,SUNGUSUNGU WAUA MWANAMKE KAHAMA

NB HII NI PICHA YA SUNGUSUNGU KIJIJI CHA BUBALE WILAYA YA SHINYANGA SIO WA KAHAMA

Modesta Kazimoto (50) mkazi wa kijiji cha Nonwe kata ya Ubagwe wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kikatili  kwa kukatwa panga kwa shoka kichwani na kundi la watu wakiongozwa na viongozi wa jeshi la jadi sungusungu wa kijiji hicho.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa nane usiku ambapo watu hao walimvamia mwanamke huyo, akiwa amelala nyumbani kwake kisha kumuua kwa kumkata kwa shoka kichwani upande wa kushoto na kumvunja mkono wa kulia .
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla amesema watu hao pia walichoma nyumba tatu na chanzo chake ni imani za kishirikina                    

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527