MAFUNZO YA SIKU 4 KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU,DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA YAANZA KATIKA UKUMBI WA DIAMOND FIELDS HOTEL MJINI SHINYANGA

Kulia ni meneja Radio Kahama Marco Mipawa akifuatilia kwa umakini zaidi  kuhusu haki za binadamu ,demokrasia na  utawala bora mapema leo katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel Mjini Shinyanga,katikati ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga,Shija Felician,pembeni yake ni mwakilishi wa ITV na Radio one,bwana Stephen Wang'anyi

Kulia ni Nunu Abdul kutoka Radio Faraja,katikati Editha Edward wa gazeti la Mtanzania,akifuatiwa na Patrick Mabula wa gazeti la majira wakifuatilia mafunzo hayo yenye lengo la kuwaongezea ujuzi katika mambo ya haki za binadamu,demokrasia na utawala bora ambayo yamefadhiliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini(UTPC)

Kulia ni Suzy Butondo wa Gazeti la Mwananchi,akifuatiwa na Kareny Masasy,katibu klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,pia mwandishi gazeti la Habari leo


Mwezeshaji,ambaye ni mwandishi wa habari mwandamizi,pia mwanasheria Juma Thomas akiendelea kutoa somo kwa waandishi wa habari 18 wa mkoa wa shinyanga


Kushoto ni Sam Bahari mwandishi wa habari mkongwe,gazeti la Mtanzania,katikati ni Ali lityawi wa Tanzania Daima wanaandika mawili matatu
Bwana Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo akitafakari jambo

Kushoto ni mkurugenzi wa malunde1.blogspot.com,na mwandishi gazeti la Zanzibar Leo bwana Kadama Malunde,katikati Lucy Masalu kutoka Radio Faraja na Geni Elias pia kutoka Radio Faraja ya mjini Shinyanga wakifuatilia mafunzo

Kulia ni Stella Ibengwe,mweka hazina SPC lakini pia mwandishi gazeti la Tanzania Daima,pembeni ni Bi Zuhura Waziri,mratibu SPC na mwakilishi Clouds media

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527