MWALIMU AUA JAMBAZI KWA MKUKI KISHAPU

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla
Siku chache tu baada ya hakimu kunusurika kufa baada ya kuchomwa kisu na mlalamikaji katika kesi moja ya baiskeli mjini Shinyanga,tukio jingine limejitokeza ambapo safari hii mwalimu wa shule ya msingi Mihama katika kijiji cha Mihama wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ameua mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni jambazi kwa kumchoma mkuki kifuani baada ya jambazi huyo akiwa na wenzake kuvamia nyumbani kwa mwalimu huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea juzi  majira ya saa saba usiku ambapo mwalimu wa shule ya msingi Mihama,aliyejulikana kwa jina la Paulo Nahembe(40) akiwa amelala nyumbani kwake alivamiwa na watu hao wakiwa na marungu,mapanga na mikuki.

Kamanda huyo ameiambia malunde1.blogspot.com kuwa Mwalimu  Paulo Nahembe alianza kupambana na watu hao na kufanikiwa kumchoma mkuki mmoja wao ambaye hakufahamika jina lake mara moja mwenye umri kati ya miaka 30-35 na akafariki dunia papo hapo huku wenzake  wawili wakifanikiwa kutoroka na jeshi la polisi mkoani Shinyanga linaendelea kuwatafuta watu hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post