ASASI YA YHDA YA SHINYANGA YAENDESHA MJADALA WA RASIMU YA KATIBA MPYA TINDE -SHINYANGA
Mwanasheria wa wilaya ya Shinyanga Saleh Hassan akitoa mwongozo kwa wakazi wa Kijiji cha Tinde katika kata ya Tinde mapema jana katika Ukumbi wa TRC uliopo eneo hilo karibu na shule ya msingi Tinde ambapo alisema mjadala utalenga zaidi aina ya muungano ambao wananchi wanautaka,ambapo mjadala utadumu kwa muda wa siku tatu yaani Agust 26 hadi 28 mwaka huu.

Wakazi wa Tinde waliojitokeza katika mjadala wa rasimu ya katika mpya ambapo pamoja na mambo mengine walipendekeza katiba itaje wazi kuwa ndoa za jinsia moja ni marufuku

Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake kuhusu aina ya muungano inayotakiwa ambapo alipendekeza kuwepo serikali tatu kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu ya katiba mpya 2013.

Mratibu wa asasi ya kiraia
Youth Health and Development Association YHDA,bwana Rigobert Rweyombiza aliwataka washiriki katika baraza hilo kutoingiza itikadi za kisiasa au dini kwani katiba itakayopatikana ni kwa maslahi ya watanzania wote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments