WAZAZI WATWANGANA MAKONDE NA KUUA MTOTO WAO

Polisi mkoani Rukwa inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wao wakati wanapigana kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa polisi Mkoa Rukwa, Jacob Mwarwanda amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Julai 22, saa 5:30 za usiku baada ya Livinus Choma(31) na mkewe  Grace Choma(28) ambao wote wakazi wa Malangali kugombana usiku.

Amesema baada ya mume na mke kurejea nyumbani ulizuka ugomvi baina yao huku mwanamke akimtuhumu mume wake kwamba anauhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine na kusababisha waanze kupigana.

Wakiwa wanapigana ghafla mume alimsukuma mke wake ambapo alitereza na kuanguka kitendo kilichosababisha kumlalia mtoto wao aitwaye Esther choma(2)  ambaye alipoteza fahamu hali ambayo wazazi hao walijua wamemuua mtoto wao huyo.

Baada ya mtoto kupoteza fahamu wanandoa hao walichukua mwili wa mtoto huyo na kwenda kuutelekeza katika nyumba ya jirani yao na kisha kupiga simu kwa diwani wa kata hiyo wakidai kuwa mtoto wao amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Diwani huyo alimtaarifu Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na kushirikiana na wazazi hao kuanza kumtafuta mtoto huyo na walimkuta pembeni ya nyumba ya jirani yao akiwa hai, lakini amepoteza fahamu.

Kutokana na hali hiyo walimpeleka katika Hospitali ya Mkoa iliyopo Sumbawanga na kuanza kupatiwa matibabu, lakini alifariki siku iliyofuata kutokana na mauvivu makali aliyoyapata baada ya kuangukiwa na mama yake.

Kutokana na kifo hicho polisi iliwashikila wazazi hao na baada ya kuhojiwa ndipo mama wa mtoto huyo alipoelezea chanzo cha kifo hicho na kudai kuwa walimpeleka mtoto huyo na kumtelekeza kwa jirani ili isijulikane kuwa wao ndiyo waliosababisha kifo hicho na pengine jirani huyo angetuhumiwa kumuiba mtoto huyo na kumuua.

Kamanda Mwarwanda alisema kuwa baada ya upelelezi kukamilika wazazi wa mtoto huyo watafikishwa mahakamani ili wakajibu mashtaka yatakayo wakabiri kufuatia tukio hilo.
source-Mpekuzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post