MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ALLY NASSORO RUFUNGA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA SHINYANGA


                                                                                                                                                                       
Huu ni mnara wa mashujaa uliopo eneo la mazingira senta mjini shinyanga eneo ambalo leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya mashujaa wa Tanzania kimkoa ambapo viongozi mbalimbali wa serikali,viongozi wa dini,wadau na wananchi wenye mapenzi mema wamehudhulia  maadhimisho hayo wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa shinyanga mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga

Viongozi mbalimbali wa mkoa wakiwa eneo la mnara wa mshujaa wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa kimkoa mapema leo

Viongozi mbalimbali mbele ya mnara wa mashujaa tayari kwa kuweka silaha za jadi na mshada ya maua ili kuwakumbuka mashujaa waliokufa kwa ajili ya watanzania

Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiweka mkuki na ngao katika eneo la mnara wa mashujaa

Mzee Mungo Mbushi mkazi wa shinyanga mmoja ya mashujaa wa tanzania baada ya kuweka silaha ya jadi

Mkuu wa wilaya shinyanga Anna rose Nyamubi  akijiandaa kuweka shada la maua

Aliyeshikilia shada la maua ni mkuu wa wilaya ya kishapu Wilson Nkhambaku

Katikati ni mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa kimkoa ambapo aliwataka wahusika kuboresha eneo la mnara wa mashujaa ili livutie zaidi.Kushoto ni mzee Mungo Mbushi mmoja wa mashujaa wa tanzania,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments